JUZI CLOUDS FM TULIKUWA KIGOGO KUTOA CHOCHOTE KWA WENZETU WALIOKUMBWA NA MAFURIK

Vituo vipo vingi lakini sisi tulienda kigogo na tulikuta vitu mbalimbali vilivyoletwa na watu au mashirika mbalimbali. Tuliwapelekea ndoo,mabeseni,dawa za meno,mafuta,sabuni,nguo,godoro,maji ya kunywa,juice na biscuit kwa watoto,malapa na vyandarua.Ila tukaja kugundua wanawake wengi wana uhitaji wa taulo za kike(pads) na nguo za ndani.Kwa hiyo wengine mtakaofatia kupeleka misaada mnaweza kuangalia na eneo hilo mnalisaidia vipi.
Tulikuta watu wengi wanafua nguo zao baada ya kuletewa maji yale ya kwenye magari.
Pia chakula cha mchana kilikuwa kinapikwa japo wanalalamika wakati mwingine watu kama wazee kukosa chakula maana hawana nguvu za kupanga foleni.Na pia wazamiaji wanasababisha wale walengwa kukosa chakula.

Doreen na mtoto
Ruben na mtoto Sabrina ambae anaumwa kifua sababu ya kulowana na mvua na maji ile juzi,pembeni ni Khadija Mwanamboka.
Mtoto huyu ana miezi miwizi mama yake wakati wa kujinusuru ilibiri ambebe kwenye pochi kubwa ili kumnusuru.
Mh.Iddi Azan mbunge wa Kinondoni alikuwa akitupa maelezo kuhusu swala la vyoo lilivyokuwa na changamoto kwa vituo vingine kasoro hapo.Maana shuleni hapo kuna vyoo angalau pamoja na vyoo vya msaada vile ya mobile.

Baada ya kukabidhi msaada tukaanza kuzungukia kuona nyumba zilivyoathiriwa na mvua na mafuriko.
Picha na Dina marios
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: