Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai, na
Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Indiana Kitivyo cha Swahili Flagship
Center, Dk. Alwiya.S. Omar, wakibadilishana mikataba baada ya kutiliana
saini ya makubaliano ya ushirikiana baina ya vyo hivyo viwili.
Mkurugenzi
wa Chuo Kikuu cha Indiana cha Marekani Kitivyo cha Kiswahili Flagship
Center, Dk. Alwiya.S.Omar, akitowa maelezo ya vitabu vya kufundishia
Kiswahili karika chuo chao, baada ya kumkabidhi Makamu Mkuu wa SUZA
Profesa Idris Ahmad Rai,
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai,
akitiliana saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kutowa mafunzo ya
Kiswahili, na Mkurugenzi wa Chuo cha Indiana cha Marekani, Kitivyo cha
Swahili FlagshipCenter Dk. Alwiya.S.Omar, utilianaji wa saini hiyo
umefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Suza Majestik Zanzibar.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai, akitowa
maelezo jinsi ya nyanja za ushirikiano baina ya vyo hivyo viwili baada
ya kutiliana saini, makubaliano hayo yaliofanyika katika ukumbi wa
Chuo hicho Majestik Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Chuo Kikuu cha Indiana Kitivyo cha Kiswahili Flahship Center. Dk
Alwiya .S.Omar, akielezea ushirikiano wa pande hizo mbili jinsi ya
kutowa elimu ya kujifunza kiswahili kwa wanafunzi wa Indiana na
kubadilishana Walimu wa Kiswahili wa vyoo hivyo viwili.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Utawala Dk. Ahmada Hamad Khamis, akitowa shukrani
kwa niaba ya Chuo chake katika sherehe za utilianaji wa saini na Chuo
cha Indiana cha Marekani katika nyenja za Elimu ya Kiswahili.
0 comments:
Post a Comment