Umoja
wa wafanyakazi wanawake wa Airtel ujulikanao kama Airtel Divas umejitoa
kuwasaidia na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania
(SWAUTA ) kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
hao wa Airtel walifanya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas na kualika
kikundi cha SWAUTA kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wafanyakazi wa
Airtel na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuwa na banda lao katika
maonyesho ya 38 ya kimataifa ya SABASABA.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo Meneja Rasilimali watu Sophia Melamali alisema”
tunayofuraha kuzindua rasmi Airtel Divas mpango maalumu wenye lengo la
kuwainua na kuwahamasisha wanawake na wafanyakazi wa Airtel kuzifikia
ndoto zao. Kama tunavyofahamu wanawake wanayo majukumu makubwa ya
familia na kazi, hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kugawa muda wao kwa
ufanisi. kwa kupitia Airtel Divas tunashirikiana kwa pamoja kupeana
ujuzi na mawazo ya namna ya kupambana na changamoto hizi na kufikia
mafanikio katika malengo tuliyojiwekea
Sambamba
na hilo tunawahamasisha wanawake kushiriki katika kujitolea na kutoa
msaada kwa jamii na ndo maana leo tumewaalika kina mama hawa wenye
ulemavu na kuwapa nafasi ya kuuza bidhaa zao na kiasi cha pesa
watakachopata leo tutakiongeza mara mbili na kuwawezesha kupata fedha za
kutosha kulipia banda katika maonyesho ya sabasaba. Tunaamini kwa
kufanya hivi tutawawezesha kukuza biashara yao. Natoa wito kwa
watanzania watakaopata nafasi ya kwenda kwenye maonyesho haya wapate
nafasi ya kuwatembelea na kuwaaunga mkono pia.
Akiongea
mara baada ya kukabithia msaada huo mwenyekiti Kikundi cha Sauti ya
Wanawake wenye Ulemavu Tanzania SWAUTA bi Stella Jairosi Alisema,
Tunawashukuru Airtel kwa kutuwezesha kupata banda zuri liliopo eneo zuri
katika maonyesho ya Sabsaba, kwa miaka 8 sasa tumekuwa tukishiriki
katika maonyesho haya lakini hatukuwahi kuwa na banda letu wenyewe.
Kupitia msaada huu kutoka Airtel kutatupatia mwanya wa kuonyesha bidhaa
zetu na kupata mwaya wa kuuza kwa soko la ndani na la nje na pia
kutatusaidia kuuza bidhaa zetu kwa kiasi kikubwa na kuongeza pato letu
na hivyo kuendeleza miradi ambayo hatukuweza kuifanya kutokana na uhaba
wa fedha.
Kwa
upande wake mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura
Muro alisema“ nimejisikia furaha kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo
na napenda kuwapongeza sana Airtel Divas kwa kujitolea kusaidia jamii
kupitia shughuli hizi za huduma kwa jamii wakiwemo wa mama hawa wa
kikundi cha walemavu nawahamasisha muendelee na juhudi hizi.Pamoja na
hayo pia nachukua nafais hii kuwahimisha Airtel Divas kufanya kazi kwa
bidii na kuonyesha uwezo wao katika maeneo yao ya kazi ili waweze kupata
nafasi nyeti katika Uongozi.
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro
(kushoto), huku akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake
wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Happy John wakikata keki
kuashiria uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel
iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania
(SWAUTA), kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili
kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba). Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Divas.
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (wa
pili kulia), akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA ) cha Kinondoni, kabla
ya kuzindua rasmi Kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza
bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao
lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Kushoto ni mwanachama wa Swauta, Adelina Mluge.
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na kikundi cha Sauti ya Wanawake
wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa Airtel Divas, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa
zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo
katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro
(kushoto), akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde
(kulia), baada ya kutembelea bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kabla
ya kuzindua rasmi Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza
bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao
lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Mgeni
Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro,
akifurahia zawadi ya kitenge baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (kulia), katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania
‘Airtel Divas’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya
Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao
kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo
katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
0 comments:
Post a Comment