Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo
(kulia) akimkabidhi nakala za jarida la utekelzaji wa shughuli za
baraza la wafanyakazi Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) , Dk Adolf Rutayuga kwenye hafla ya uzinduzi
wa baraza hilo la kwanza la wafanyakazi wa NACTE jijini Dar es Salaam
leo Oktoba 4, 2016. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE,
Mhandisi, Stephen Mlote.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo
(katikati) akizungumza na wafanyakazi wakati akizindua baraza la
kwanza la wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ,
jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2016. Kulia ni Kaimu Katibu
Mtendaji wa NACTE, Dk Adolf Rutayuga na kushoto ni Mwenyekiti nwa Bodi
ya NACTE, Mhandisi Stephen Mlote
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo
(kulia) akizindua baraza la kwanza la wafanyakazi wa Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es Salaam jana. na kushoto ni
Mwenyekiti nwa Bodi ya NACTE, Mhandisi Stephen Mlote.
Wafanyakazi
wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakimsikiliza kwa makini Naibu Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ambaye alizindua bara za kwanza la
wafanyakazi wa NACTE jijini Dar es
Salaam leo Oktoba 4, 2016.
Na Mwandishi Wetu
Taasisi
ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ina dhamana kubwa ya
hatma ya Elimu ya Ufundi nchini Tanzania, jambo linafanya elimu ya
Ufundi kuwa ya umuhimu hususan katika kipindi hiki ambacho agenda kuu
ya Taifa ni kujenga Uchumi wa Viwanda kwakujenga elimu ya ufundi
imara.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Sayansi na
Teknlolojia, Dk Leonard Akwilapo wakati akizindua baraza la wafanyakazi
wa NACTE jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4,2014.
Dk Akwilapo alisema kuwa agenda hiyo inabidi ichukuliwe na Baraza hili kama kigezo cha kupima utendaji wa kazi wa NACTE.
“ Ni
matumaini yangu kuwa wajumbe wote wa Barza hili tunalolizindua leo
watatambua hili na kutoa mchango maridhawa katika Maendeleo ya Taifa na
kufanikisha agenda ya Taifa ya “Uchumi wa Viwanda”.alisema naibu katibu
mkuu huyo
Alisemama
kwa sasa i uchumi wa dunia unaendeshwa katika misingi ya soko huria na
Sekta yetu ya Elimu haijaachwa nyuma katika hilo. Hata hivyo kwa kiasi
kikubwa utoaji wa Elimu nchini kwetu bado ni huduma.
Hivyo
basi NACTE lazima iwe makini katika kusimamia uendeshaji wa Sekta hii,
kwa kuzingatia maadili ili kuondoa huo utata. Endeleeni na usimamiaji
madhubuti wa Elimu ya Ufundi, msiyumbishwe na wafanyabiashara wanaotaka
kuharibu mfumo wetu wa elimu.
Matarajio yenu yaendelee kuwa ni utoaji wa elimu yenye ubora wa kiwango cha juu cha mafunzo.
“Ni
RAI yangu kwa Baraza la Wafanyakazi kusimamia hili kwa nguvu zenu zote.
Msiposimama imara mtakuta mna vyuo batili, vyuo vinavyoendesha mafunzo
kiholela bila kufuata taratibu, na vitatoa wataalamu wasio na uwezo
unaolingana na kiwango cha vyeti wanavyotunukiwa. Baraza la Wafanyakazi
hamtakwepa lawama katika hali kama hiyo” alisema Dk Akwilapo
Alisema
kuwa uzinduzi wa baraza hilo lilikuwa ni muhimu sana katika historia
ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), hii ni kwa sababu kama
taasisi mmekuwa hamna Baraza la Wafanyakazi kwa kipindi kirefu sana.
Natambua kwamba kwa kipindi chote cha uhai wa taasisi tangu ilipoanza
shughuli zake takribani miaka kumi na tano (15) iliyopita, mmekuwa
mkiendesha shughuli zenu bila kuwa na chombo hiki. Na hiyo ni kinyume
kabisa na taratibu za utawala bora. Sina budi kuwapongeza kwa kutambua
hilo na kuamua sasa kuanza kutekeleza majukumu yenu kulingana taratibu.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa alifahamu kuwa nia na juhudi za kutaka
kuunda Baraza la Wafanyakazi la Taasisi hii zilianza muda mrefu yapata
miaka nane (8) iliyopita.
Changamoto
iliyokuwepo na kukwamisha uundwaji wa Baraza hili muhimu ilikuwa ni
kutokuwepo kwa tawi la chama cha Wafanyakazi katika Taasisi hii.
Utaratibu wa kuundwa kwa Baraza la Wafanyakazi unahitaji kuwepo na
makubaliano ya pande mbili, upande wa Mwajiri kwa upande mmoja na Chama
cha Wafanyakazi mahali pa kazi kwa upande mwingine. Kwa sasa hali ni
tofauti kwa kuwa “TUGHE” moja ya chama cha Wafanyakazi nchini
kimefanikiwa kuanzisha tawi lake hapa na hatimaye kuwezesha kuundwa kwa
Baraza hili la Wafanyakazi.
“Kwa
kutambua hili napenda nichukue fursa hii kulipongeza Baraza la Uongozi
wa NACTE na Menejimenti yake kwa jitihada mlizozifanya kuhakikisha kuwa
tawi la chama cha Wafanyakazi “TUGHE” linafunguliwa hapa na kisha kuunda
Baraza hili la Wafanyakazi. Baraza ambalo kuanzia leo linakuwa rasmi”,
alisema Dk Akwilapo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi wa NACTE, Mhandisi, Stephen Mlote
alitaja majukumu ya baraza la wafanyakazi kuwa ni pamoja na
kuwashirikisha wafanyakazi wa NACTE katiak utekelezaji wa shughuli za
NACTE kwa kushirikiana na uongozi.
Majukumu
mengine ni kushauri NACTE juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa
kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa huduma zitolewazo na NACTE ni za
kuridhisha na zimo katika lengo la kujenga Taifa.
Mwenyekiti
huyo alitaja majukumu mengine ya baraza hilo ni kushauri NACTE juu ya
mambo mengine muhimu yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment