BENKI YA NBC TANZANIA YAWAFUTURISHA VIONGOZI MBALI MBALI

IMG_2688 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza wananchi mbali mbali walioalikwa katika  futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana. IMG_2703 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bibi Mizinga Mellu,(wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi Mwanaidi (kulia) . IMG_2735 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,Bibi Mizinga Mellu,akizungumza machache na kutoa salamu za Uongozi wa Benki hiyo wakati wa futari waliyoiandaa kwa wananchi wa Zanzibar jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,Wilaya ya Magharibi Unguja. IMG_2746 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(katikati) na makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,(kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bibi Mizinga Mellu,na (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi Dk.Mussa Assad. IMG_2760 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,akisoma Dua baada ya kumalizika kwa  futari iliyoandaliwa na  Benki ya NBC katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,kwa Wananchi wa mbali mbali na wateja wa Benki hiyo upande wa Zanzibar. IMG_2769Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(kushoto) akisindikizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bibi Mizinga Mellu,baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: