Na Anna Nkinda – Maelezo, Mafia
Wazazi
na walezi wilayani Mafia wametakiwa kutokubali kupokea mahari za
watoto wao wakiwa wanafunzi bali wawasimamie na kuhakikisha wanasoma
kwa bidii na kufika elimu ya chuo kikuu.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na
wanafunzi pamoja na wazazi wa shule ya Sekondari Bweni iliyopo kata ya
Kanga wilaya ya Mafia mkoani Pwani.
Mama
Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
alisema baadhi ya wazazi wanapokea mahari za watoto wao na kuwaozesha
wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huwafanya kukatisha masomo yao na
wanawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu.
“Mtoto
akisoma atakuwa na maisha mazuri hapo baadaye ataweza kufanya kazi za
kitaalamu za kuajiriwa au kujiajiri yeye mwenyewe, kujikomboa na
umaskini, kuwasaidia wazazi wake, ataepukana na mimba za utotoni na
kujiepusha na maradhi yanayotokana na ngono zembe kwani elimu ni
msingi wa kila kitu”.
Wanawake
wenzangu mtoto wako wa kike akiwa mwali usikubali kumuweka ndani ili
asubiri mwanaume wa kumuoa na ukisikia mmeo kapokea mahari ili binti
huyo aolewe katoe taarifa sehemu inayohusika ili sheria iweze kuchukua
mkondo wake”, alisisitiza Mama Kikwete.
Kwa
upande wa wanafunzi aliwaasa kujiepusha na kitendo cha kujiingiza katika
mapenzi wakiwa na umri mdogo bali wasome kwa bidhii , wawe na nidhamu
kwa walimu wao na kuwa na malengo katika maisha yao kwa kufanya hivyo
watatimiza ndoto zao.
Alisema,
“Wanangu someni kwa bidii msitake utajiri wa haraka, watoto wa kiume
mnaacha kwenda shule, mnakatisha masomo na kukimbilia kuvua samaki kwa
kudhani kuwa mtapata maendeleo kumbukeni elimu ni urithi usioweza
kutoweka katika maisha yenu”,.
Aidha
Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwahimiza wazazi kwenda Hospitali kupima
ugonjwa wa saratani za shingo ya kizazi, matiti na tezi dume ambazo
zikigundulika katika hatua ya awali mgonjwa anaweza kutibiwa na kupona
kabisa.
Kuhusu
utunzaji wa ardhi Mama Kikwete alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na
ardhi nzuri yenye rutuba inayowavutia watu wengi na kuwasihi wananchi
kutoiuza kiholela bali waitunze, kama kuna wawekezaji utaratibu maalum
ufuatwe.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndekilo aliwahimiza wananchi hao
kuona umuhimu wa kuwarithisha watoto wao elimu ambayo ni ufunguo wa
maisha na siyo mali kama uvuvi, ng’ombe na mashamba.
Eng.
Ndekilo alisema atakuwa mkali kwa mtu yoyote atakayekatisha elimu ya
mtoto wake na katika suala la mtoto kuacha shule baada ya kupewa
ujauzito mahakama ndiyo itakayotoa maamuzi na siyo wazazi kumalizana
wenyewe kwa wenyewe.
Akisoma
taarifa ya shule Mwalimu mkuu Mohamed Msossow alisema shule hiyo
ilifunguliwa mwaka 2007 ikiwa na walimu wanne na wanafunzi 199 kati ya
hao wavulana walikuwa 147 na wasichana 52 . Hivi sasa kuna walimu 20 na
wanafunzi 131 kati ya hao wavulana 61 wasichana 70 na walimu 20.
Aliyataja mafanikio waliyo nayo ni walimu wa kutosha wa masomo ya sanaa,
vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi na sanaa kwa uwiano wa
mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja, madarasa ya kutosha, ushirikiano
mzuri na jamii inayowazunguka na matokeo mazuri ya kitaaluma katika
mitihani ya kidato cha pili na cha nne.
“Changamoto
zinazotukabili ni upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati,
nyumba za walimu na vifaa vya maabara, kutokana na mazingira ya mahali
shule ilipo shule inahitajika kuwa na usafiri ili kurahisisha walimu
kufika wilayani”.
Idadi
ndogo ya wanafunzi inayosababisha kupata mgao mdogo wa fedha ya ruzuku
kutoka Serikalini na kusababisha ugumu katika kuendesha shughuli
mbalimbali za shule, ukosefu wa umeme na uhaba wa vyanzo vya
maji”,alisema Mwalimu Msossow.
Mama Kikwete yuko wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na
akiwa shuleni hapo aliwapatia wanafunzi zawadi ya shilingi milioni
moja.
Shule
ya Sekondari Bweni imejengwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kisiwa cha
Mafia (MIDEF) chini ya usimamizi wa Dkt. Ramadhan Dau ambaye ni
Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuikabidhi
kwa Serikali ambapo hivi sasa ni Shule ya Sekondari ya kata ya Kanga.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia
Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia
kuanza ziara ya siku mbili wilayani humo tarehe 13.3.2015
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mwalimu Mariam Halfan
Haji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kama ishara
ya upendo na kumkaribisha rasmi kutembelea wilaya ya Mafia tarehe
13.3.2015
Akina
mama wa Mafia waliofika kumpokea Mama Salma Kikwete wakati akiwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Mafia wanaonekana wakiwa wamebeba mabango ya
kumkarisha wilayani humo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau alikuwa ni
miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika kwenye uwanja wa ndege wa
Mafia kwa ajili ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili
wilayani humo tarehe 13.3.2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi/albino aliyekuwa amebebwa na mama yake. Mama Salma alikutana na
mtoto huyo wakati alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau akitoa
maelezo mafupi kuhusu Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya
Kanga wilayani Mafia ambayo imejengwa na “Mafia Island Development
Foundation, MIDEF”. Dkt. Dau ni mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo. Mama
Salma alitembelea Shule hiyo tarehe 13.3.2015. Waliokaa kutoka kushoto
ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Injinia Evarist Ndikilo, Ndugu Mohamed Msosa, Mwalimu Mkuu wa Shule
hiyo na mwisho ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mafia.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia tarehe
13.3.2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni
katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana
naye.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni
katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana
naye.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni
katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana
naye.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama
wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama
wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama
wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari
Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari
Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi. PICHA NA JOHN
LUKUWI
0 comments:
Post a Comment