Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba, Arden Kitomari,akitoa mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt Sadaka Gandi.
Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference & Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa na taratibu zake
Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii aliyesajiliwa
Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo, Habari, na Wajasiriamali mashughuri
Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.
Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa Shear Illusions
Baada ya mada zote kukamilika, wadau walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo iliyoandaliwa
Huu ukawa wakati muafaka wa wasanii kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na afisa kutoka BASATA
Mwanahabari Maimuna Kubegeya hakuwa nyuma kuuliza maswali na kufahamiana na CEO wa COSOTA, Ms Doreen Anthony Sinare
MwanaBlog maarufu John Bukuku akifurahia jambo na Meneja Masoko wa NHC, Arden Kitomari
Antu Mandoza akisisitiza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Popular Links ambao ndio waandaaji wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka Clouds Media
Warembo katika picha ya pamoja
Wasanii wa kutengeneza muonekano kutoka LuvTouch Manjano ya Shear Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup
Mariam Ndabagenga, Mkurugenzi wa Popular Links akitoa neno la Shukran kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.
Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt, Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds Media na Slide Visuals.
0 comments:
Post a Comment