Na Athumani Issa, Hanang'
MWANARIADHA
mkongwe nchini, Wilhelm Gidabuday, ametangaza rasmi nia ya kugombea
Ubunge katika Jimbo la Hanang’ kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Gidabuday
ambaye katika siku za hivi karibuni, amejozelea umaarufu kutokana na
misimamo yake ya kutetea masilahi ya wanariadha nchini, aliyabainisha
hayo juzi katika mazungumzo maalum na Wazalendo 25 Blog.
Alisema
baada ya kufikiria kwa makini huku akifuata ushauri wenye busara kutoka
kwa wenyeji wa wilaya ya Hanang’, ameamua kuitikia maombi ya wana
Hanang.
“Baada
ya kufikiri na kushauriwa vizuri na watanzania wenye busara wenyeji wa
Hanang’ hatimaye nimeamua kutangaza nia yangu ya kuwania nafasi ya
Ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015 kupitia Chadema”, alisema Gidabuday.
Gidabuday
alisisitiza kwamba uamuzi wake kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo,
ambalo kwa sasa linashikiliwa na Dkt. Mary Nagu (CCM), umetokana na
imani kwamba kugombea nafasi yoyote ni haki ya msingi ya kila Mtanzania
kikatiba.
“Kabla
ya kujitathmini mwenyewe nilifanyiwa tathmini na rika tofauti ndani ya
jamii, makundi hayo yakiwakilisha watu wenye busara katika jamii. mimi
nilikumbushwa nijitathmini baada ya wao kuniweka katika orodha ya watu
wenye sifa stahiki”, alisema.
Alipoulizwa kuhusu uwezo wake katika kutumikia nafasi hiyo, Gidabuday alisema uzoefu wake katika kupigania maendeleo ya michezo nchini kunampa kiburi kuwa akipewa fursa hiyo atawatumikia wananchi wa jimbo lake.
Alipoulizwa kuhusu uwezo wake katika kutumikia nafasi hiyo, Gidabuday alisema uzoefu wake katika kupigania maendeleo ya michezo nchini kunampa kiburi kuwa akipewa fursa hiyo atawatumikia wananchi wa jimbo lake.
“Wanaonifahamu watanijibia hili, mwaka 2010, niliongoza harakati za kuwaondoa wavamizi wa vyanzo vya maji pembezoni mwa mlima Hanang, upande wa kijiji cha Nangwa, utakumbuka wavamizi wale walijiamini sana sababu kati yao kulikuwa na wajomba zake Mbunge”, alisema Gidabuday.
Katika
siku za hivi karibuni, kutokana na misimamo yake na harakati za kupinga
rushwa, Gidabuday alijikutana akiingia kwenye mgogoro na viongozi wa
shirikisho la riadha nchini (RT), inayoongozwa na Mbunge wa Mvomero,
Anthony Mtaka (CCM).
Mwanaharakati
amekuwa akiutuhumu uongozi wa RT, kuhusika na michezo michafu ambayo
imepelekea mafanikio kiduchu ya Riadha, alisema kazi yake ya kwanza kama
Mbunge itakuwa ni kumaliza migogogro ya ardhi kati ya wakulima na
wafugaji Jimboni mwake.
“Nitahakikisha
natatua tatizo la migogoro ya ardhi yaliyoanza tangu uvamizi wa
mashamba ya Gehandu na Bassotu mwishoni mwa 1960 hadi mwanzoni mwa 1980
kwa kile kilichodaiwa kuwa uwekezaji wa shirika la NAFCO la Canada,
kufuatilia kesi iliyopo mahakama ya dunia kuhusu haki ya jamii ya
Wadatoga maarufu Wabarbaig”, alisema
Aidha mwanariadha huyo ambaye kwa sasa anaendesha mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha michezo cha kitaifa (National Sports Village), alisema akiwa Mbunge atahakikisha ujenzi wa kituo hicho ambacho kimekuwa kikiwekewa pingamizi kutokana na mitizamo mbalimbali na tamaa ya wachache, kinakamilika.
Aidha mwanariadha huyo ambaye kwa sasa anaendesha mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha michezo cha kitaifa (National Sports Village), alisema akiwa Mbunge atahakikisha ujenzi wa kituo hicho ambacho kimekuwa kikiwekewa pingamizi kutokana na mitizamo mbalimbali na tamaa ya wachache, kinakamilika.
Mwanariadha
huyo, alisema msukumo wa kuingia bungeni unatokana na hamu ya kuona
rasilimali nyingi za wilaya ya Hanang’ zinatumika kuwakomboa wana
Hanang’ kuondokana na lundo la umasikini unaowakabili kwa sasa.
“Wilaya
ya Hanang ni tajiri sana, ardhi yenye rutuba, mlima wa tatu kwa urefu
Tanzania, msitu wenye wanyama adimu duniani (Extinct & Rare Birds),
ziwa la chumvi, mifugo na mazao mengi sana! Iweje wanahanang wanaishi
maisha wanayoishi sasa kama si uzembe wa viongozi wasio wazalendo?”
alihoji
0 comments:
Post a Comment