Mhandisi Kisaka kutoka TCRA makao makuu akitoa somo kwa viongozi wa vyombo vya habari kanda ya Nyanda za juu kusini.
Na Edwin Moshi, Mbeya
Vyombo
vya habari nchini vimetakiwa kuwa makini na kuripoti habari za uchaguzi
mkuu wa mwaka huu kufuata maadili na weledi wa taaluma hiyo ili
kufanikisha uchaguzi huo kwa amani
Hayo
yamesemwa leo jijini Mbeya na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA
wakati wakiwapa semina mameneja na wamiliki wa vyombo vya habari
vilivyopo kanda ya nyanda za juu kusini semina iliyofanyika jijini Mbeya
Akizungumza
katika semina hiyo wakati wa hotuba ya kufungua semina hiyo Naibu
Mkurugenzi idara ya utangazaji TCRA makao makuu Bw. Fredrick Ntobi
amewasisitiza waandishi wa habari kote nchini kuhakikisha wanafuata
maadili ya kazi zao ili kuepuka madhara yatakayoweza kujitokeza pindi
watakapotoa taarifa potofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi
nyingine zitakazofuata baada ya uchaguzi huo
"Naomba
muwe makini na uandishi wenu wa habari maana ninyi ninyi ndio
mtakaofikishwa mahakamani, ninyi ndio mtakaofikishwa The Heag, ajirini
watu wenye professional (taaluma) ya habari, hii itasaidia kuepuka kauli
za uchochezi, zitawamaliza na niwahakikishie sisi kama mamlaka tupo
makini na tutafuatilia vyombo vyote vya habari" amesema Ntobi
Kwa
upande wake Mhandisi mkuu idara ya Utangazaji TCRA makao makuu Mhandisi
Andrew Kisaka amewataka washiriki kuhakikisha wanazingatia usawa katika
kutoa taarifa za uchaguzi na kuepuka upendeleo wa baadhi ya vyama
"Unakuta
CHADEMA mnawapa dakia mbili kujieleza halafu CUF mnawapa dakika 20 hili
sio sawa, hakikisha mnatoa kipindi kilichowapa fursa sawa wagombea wote
bila upendeleo
Aidha
Kisaka amewaonya waandishi wa habari kuacha kujiingiza kwenye siasa kwa
kushabikia wagombea fulani na kuingiza itikadi zao katika kuripoti
habari za uchaguzi kwa kuwa itasababisha kuwagawa wananchi na kuona
kituo chako kina upendeleo jambo ambalo halitakiwi
Katika
semina hiyo washiriki wamepewa nafasi ya kuuliza ma swali na kutoa
ushauri wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kwa lengo la kurahisisha
utekelezaji wa mambo hayo katika vyombo vyao vya habari wanavyofanyia
kazi
Semina ikiendelea
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo
Waandishi wa habari wakiandika vitu muhimu
Mwandishi wa habari akichangia mada katika semina hiyo.
0 comments:
Post a Comment