Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga
wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki
maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8
mwaka huu.
Na Andrew Chale.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara
wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara
maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu,
kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na
utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.
Nyalandu
aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga
wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki
maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata
kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
“Leo
hii tunawaaga hapa. Nyie ndio Tanzania hivyo mnapokuwa huko mjue
mmebeba watanzania wengine zaidi ya Milioni 40. Ni wakati wa kuvitangaza
vivutio na uzuri wa Tanzania na ilikuongeza soko letu la Utalii na
uwekezaji” alieleza Nyalandu.
Pia
aliongeza kuwa, Wizara yake ya Utalii itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake
yaliyokusudiwa ikiwemo kujitangaza ndani na nje ikiwemo kuendelea kuunga
mkono juhudi za kupambana na Uharamia dhidi ya meno ya Tembo, wanyama
na nyara za serikali kiwemo pembe za ndovu.
Afisa
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi (kushoto) akiwa na
Dorothy Masawe (Kulia) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,
wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akibdilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
Deputy
Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels (kulia), Afisa wa
Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion (kushoto)
wakiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa.
CEO
wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi, akisalimiana na
Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara katika sekta utalii wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na
Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion wakati
wa hafla hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na
wafanyabiashara akiwemo Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by
Hilton Bw. Florenso Kirambata ( wa pili kushoto).
Mkurugenzi
wa Biashara wa Flight Link, Bw. Ibrahim Bukenya akiwa na Deputy Head of
Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels wakati wa hafla hiyo.
Wadau wakifurahi jambo.(Picha zote na modewjiblog)
0 comments:
Post a Comment