HAKIMU FEKI AKAMATWA NA POLISI ARUSHA.



Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la Denis Paulo mkazi wa Ngorongoro amekamatwa na jeshi la polisi katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso Arusha mjini kwa utapeli wa kijifanya hakimu. Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ya mwanzo Mhe.Smaiton Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hivi karibuni na kusema kuwa mtuhumiwa huyo yupo mikononi mwa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi. Hakimu huyo amesema kuwa kuna mtu mmoja aitwae Ezekiel George ambaye ni mshtakiwa katika kesi namba 276 ambapo zipo nyingine nne ambazo zimesajiliwa,aliletwa mahabusu na ndugu yake aitwae Jakson George alifika akauliza watu waliokuwepo nje kuwa anawezaje kumuwekea ndugu yake huyo dhamana ndipo alipokutana na huyo tapeli na kumwambia ampe shilingi elfu 50,000 ataweza kumsaidia. 

Amesema kuwa kijana huyo alipiga simu kwa dada yake, ili amtumie pesa hiyo kwaajili ya kumpatia huyo tapeli, lakini kijana alistuka akaona bora aulizie zaidi ndipo akamuuliza mshauri wa mahakama ,kwamba nawezaje kusaidiwa ndipo mzee wa mahakama akamwambia mwuite aseme kuwa ni baba yake, ndipo yule tapeli akakimbia kwa kuona mbinu yake ya kujipatia fedha kwa njia isiyo halali imegunduliwa. Tapeli huyo alipoulizwa kuwa amefuata jambo gani mahakamani hapo alisema amekuja kumuwekea dhamana ndugu yake aitwae John ambapo alipoulizwa jina la pili la huyo ndugu yake akawa halifahamu ,na aliulizwa tena huyo ndugu yake ni mkazi wa Arusha alipoulizwa sehemu gani pia akawa hajui,jambo ambalo linapelekea kuonekana siyo mtu mzuri . 

Amesema kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, wao kama mahakama tayari walishaweka mtego kwaajili ya kuwanasa watu kama hawa ,ambao wamekuwa wakichafua mahakama wakamatwe na vyombo vinavyohusika na mambo hayo ,amesema kuwa tapeli huyo amekutwa na vitambulisho vine vyenye majina tofauti na alipohojiwa na polisi akaanza kuomba msamaha. 

Aidha amewataka wananchi kufahamu kuwa mahakamani hakuna maswala ya rushwa, na waendelee kuitegemea ila kuna baadhi ya watu ambao wanaotaka kuichafua , ili watu waone mahakimu na makarani huwa wanakula rushwa , amewataka wananchi kuwa makini na watu kama hao,na maswala kama hayo yanapigwa vita,ndiyo maana huyo tapeli amekamatwa.
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: