Mratibu
wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini,
Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika
hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake
walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa
zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/ wafanyewatabasamu
Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
Sanaa
tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya
watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda
kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
Sanaa
tiba ikapandisha mzuka, viganja vikazungumza kama inavyoonekana kwa
mtoto Heri. Wafanye Watabasamu inakuombea upate nafuu ya mapema.
Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico.
“Tukikosea
je?!” Swali alilouliza mtoto Clara na kuzua kicheko. Aliliuliza baada
ya mchoraji Paul Ndunguru aliyeipa kamera mgongo kusema kuwa wachore
huku wamefumba macho. Kutoka kushoto: Tatu Bendera, Mama Pili Mtambalike
na Beatrice Makelele.
Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
Kulikuwa na aina mbalimbali za sanaa tiba. Komediani Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga (kulia) alikuwa kivutio kwa watoto.
Mtoto Clara (kulia) akiwa na rafiki wa Wafanye Watabasamu, Arafa Salim.
Rafiki
wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni gwiji la uchoraji nchini, Paul
Ndunguru, akiangalia umahiri wa uchoraji wa mtoto Clara wakati wa zoezi
la sanaa tiba.
Hakika
sanaa tiba ni dawa. Mtoto Henry alidhihirisha kuwa hata naye komedi iko
damuni. Toka kulia; Abdul Kingo, Faiza Ally, Fred Halla, Wakuvwanga,
Amani Abeid na Lute Mwakisopile. (Picha zote na Wafanye Watabasamu).
Links:
0 comments:
Post a Comment