Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu
kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa
tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa
mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama
"Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa
Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili
kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye
mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi Maalumu, Trollhattan-Sweden
MGAHAWA
mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi
maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na
kuvunja rekodi ya dunia.
Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi
Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa
mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya
Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha,
alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa
hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika
katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika
uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti
wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson
walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea
kufurahishwa na juhudi za Kapande.
Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na
mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na
Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.
Alisema
Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio
tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.
Alisema
hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji
na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
"Ni
dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa
kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda
tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."
Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
Katika
mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana
na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine
katika mitandao ya wapishi wakuu.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na Afisa kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania,
Tagie Daisy Mwakawago (kulia) wakielekea eneo la tukio.
Kapande
ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu
ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani
kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza
na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.
Alisema
akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi
nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia
nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini
mchakato kamili ulianza mwaka 2013.
"Tulilazimika
kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo
walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili
kuwaje.
Kapande
ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo
kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema
amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo
ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa pili
kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi mgahawa unaotoa huduma za chakula
cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of
Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na
mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia). Wanaoshuhudia tukio hilo
ni Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto), Makamu mwenyekiti wa
kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime
Nordborg (katikati).
Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika
kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani,
baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais
wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais
mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya),
Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa
zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine
ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais
wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide,
Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca
Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea
ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine
wengi.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiongozana na
Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika
kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika
mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande
kwenye sehemu maalum aliyoandaliwa.
Pichani juu na chini ni wadau kutoka kila kona ya dunia waishio nchini Sweden walihudhuria.
Bw.
Per R. Bostrom akisalimiana na Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund
(aliyeketi). Kulia ni Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh.
Dora Msechu.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na mwenyeji
wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund wakiwa meza kuu.
Meza kuu.
Mwenyekiti
wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo
Kilumanga (katikati) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye
uzinduzi wa mgahawa huo.
Mmiliki
wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama
"Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa
Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande
akizungumza machache na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kutoa risala ya ufunguzi.
Meza kuu wakifuatilia historia ya Chef Issa Kapande (hayupo pichani) wakati akizungumza na wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akisoma risala
mara baada ya kuzindua mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania
unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food)
uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef
Issa Kapande.
Afisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini
Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago akitambulishwa kwa wageni waalikwa.
Baadhi wageni waalikwa wakisikiliza historia ya Chef Issa Kapande kabla ya mgeni rasmi kusoma risala ya ufunguzi.
Ukumbi mzima ulionekana kuvutiwa na historia ya maisha na mafanikio ya Mtanzania Chef Issa Kapande (hayupo pichani).
Meya
wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha
Chef Issa Kapande ambapo alimuomba aitafutie nafasi ndani ya mgahawa
wake kama kumbukumbu.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (kushoto) na
mwenyeji wake Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund pamoja na
Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya
Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (kulia) wakiongoza wageni waalikwa
300 kushiriki chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mmiliki wa mgahawa
huo Chef, Issa Kapande.
Chef Issa Kapande akikata nyama ya Mbuzi kwa ajili ya mgeni rasmi, Mh, Balozi Dora Msechu.
Mgeni
rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akifurahi jambo
na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent
Zanzibar, Khamis Mwinjuma Simba (kushoto).
Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund akijisevia minofu ya nyama ya Mbuzi wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo.
Wageni wakiendelea kupakua chakula.
Mwenyekiti
wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo
Kilumanga (kulia) na mkewe wakishiriki chakula cha jioni kwenye mgahawa
wa Mtanzania mwezao.
Katibu
wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kushoto)
pamoja na Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu ni miongoni kati
ya wageni waalikwa 300 waliohudhuria uzinduzi huo.
Katibu
wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kulia),
Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu (kushoto) pamoja na mtoto wa
Mwenyekiti wa chama hicho, Grace Saulli wakijichana msosi uliondaliwa
na Chef Issa Kapande.
Wageni
waalikwa wakiendelea kupiga msosi uliofurahiwa na wengi ambao utakuwa
unapatikana kwa chakula cha mchana kwa kipindi cha mwezi mmoja na hapo
baadae itakuwa mpaka chakula cha usiku ndani ya mgahawa wa "Lunch by
Chef Issa" (The house of Tanzanian food).
Mh. Balozi Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund.
Mgeni rasmi Mh. Balozi Dora Msechu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili
kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Watanzania
waishio Sweden (TANRIKS), Daniel Saulli (kushoto), Mhasibu wa chama
hicho, Emmanuel Ntundu (kulia), Katibu wa chama hicho, Mathias Pembe (wa
pili kulia) pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
Mgeni
rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kulia)
na Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha
kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of
Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa
Kapande katika picha ya pamoja kikundi cha burudani.........
Mtanzania
ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania
unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food)
uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha
ya kumbukumbu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
Afisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini
Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago, Chef Issa Kapande katika picha ya
pamoja na timu yake kwenye mgahawa huo.
Mdau Abraham Juma Ndwatta wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden akiwa na Grace Saulli kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
Wadau wakiendelea kupiga picha na Mh. Balozi Dora Msechu.
Mh. Balozi Dora Msechu akisakata rhumba kwenye uzinduzi huo.
Chef Issa Kapande akicheza muziki na wageni waalikwa.
About Unknown
0 comments:
Post a Comment