( Leo tarehe 20th 2014 ni miaka miwili
kamili imepita bila katiba mpya wala mafanikio yoyote katika mchezo wa riadha zaidi ya aibu kwa taifa letu.
( Inaelezwa kwamba mwaka mzima umetimia bila kikao
cha kamati ya utendaji kufanyika kama ilivyo sheria, kanuni na taratibu za
lazima za BMT.
( Leo hii RT imeburuzwa mahakamani (TEMEKE) kwa
kudaiwa zaidi ya TSH: 20,000,000 kwa sababu ya uzembe wa viongozi wa taasisi
hiyo isiyo na katiba inayotambulika.
( Mapema mwezi huu timu za kwenda kambini nje ya
nchi zilichaguliwa mezani badala ya kuchaguliwa viwanjani kwa vigezo vya
kushindanishwa ili walio bora wapelekwe.
Mheshimiwa waziri hata kwa macho tu hayo
yanayofanywa na viongozi wa RT huyaoni, pia waheshimiwa wa BMT kimya chenu kinampatia
nani tija?
(PICHANI)Mkurugenzi
wa Michezo (LEONARD THADEO) ndiye mvunjaji mkubwa wa sheria, kanuni na
taratibu kwani yeye ndiye anayewakingia kifua viongozi haramu wa RT pia ni yeye alisimamia uchaguzi wa MOU.
Na Wilhelm Gidabuday, mwanaharakati wa Riadha Nchini
RT yaburuzwa mahakamani, Mtaka atuhumu serikali
Laiti angejua wala asinge nena bora angepiga kimya; ‘Tangu lini serikali kwa maana ya wizara ikawa na maamuzi ya mwanariadha gani aende na yupi asiende’ RT ndiyo kiungo kati ya serikali na wachezaji.
Mwanariadha chipukizi ATSON MBUGI ambaye ni mwalimu wilayani Kilindi Tanga alijikuta akisoma jina lake kwamba yupo New Zealand wakati yeye alikuwa Kilindi akifundisha darasani.
Kocha maarufu nchini mwenye vigezo vya juu kabisa vya (IAAF) SAMWEL TUPA naye ameachwa kinyemela lakini jina lake likasomeka yupo New Zealand!
MASWALI MAZITO: Nani aliyeenda, nani alipaswa kwenda, kwa nini majina yameleta utata, kwa nini kuna usiri? Je posho zao nani kachukua?
Ni wajibu wetu kufahamu jinsi gani pesa za walipa kodi inatumika wakati kuna fungu kutoka vyama vya michezo duniani inapaswa kutumika.
Je majina yote mawili kukosewa ni bahati mbaya ama kusudi?
Je RT baada ya kushitakiwa mahakamani kwa kudaiwa zaidi ya Tsh: 20,000,000 viongozi watata na wasiojitambua wa RT wanapaswa kuendelea kujiita viongozi waadilifu wa taasisi hiyo muhimu isiyo na katiba?
‘Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michechezo wafukuze kazi Nyambui na ndugu yake wa ukoo Anthon Mtaka hata kama ni shemeji zako”
RT imekuwa kichaka cha kuchota fedha hazina na kupeleka watu baki.
Katibu wa RT anamwachia nani ofisi badala ya kumwacha kocha kwenda na timu kambini? POSHO tu ndiyo inayowazingua wa viongozi RT?
Katibu wa RT anamwachia nani ofisi badala ya kumwacha kocha kwenda na timu kambini? POSHO tu ndiyo inayowazingua wa viongozi RT?
0 comments:
Post a Comment