Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Aj It Development Bw Jackson Audiface
akizungumzia kuhusu Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali
Yatakayofanyika Mkoani Dododma Mwezi Aprili mwaka huu.Maonyesho hayo ya
kazi za Vijana wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya
Dodoma. Lengo
la Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa
Tanzania.Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana
Wajasiriamali Ili kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli
zao za Ujasiriamalia .
Baadhi
ya Bidhaa Ambazo zinazozalishwa na Vijana wajasiriamali Waliohitimu
Vyuo vikuu Mbalimbali hapa Nchini Na Ambao Bado wako Vyuoni kuendelea na
Masomo yaoamabzo zitaonyeshwa katika Maonyesho hayo Yatakayofanyika
Mkoani Dodoma Yakiwa Ni ya Tatu kuafanyika hapa Nchini kwa Lengo la
Kukuza soko la Kazi za Vijana wajasirimali pia Kuzitangaza na Kuatatua
Ngangamoto Mbalimbali Zinazowakabili Vijana wa Kitanzania Kama Vile
Vibali vya Kufanya Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali hapa Nchi.Wadau
Mbalimbali wa Vijana Mnaombwa Kujitokeza Kudhamini Maonyesho hayo.Bidhaa
Mbalimbali za Kilimo Zinazozalishwa na Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao
watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.Bw
Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika
Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana
wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao
walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya
Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana
wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Akikagua Moja ya Shuguli za Kikundi
cha Vijana kijulikanacho Kama Mae Ambao watashiriki Katika Maonyesho
hayo.
Kampuni
ya AJ IT DEVELOPMENT inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za
vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth
Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 - 5
April, 2014 Mkoani Dodoma.
Kwa
mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya AAj It Development Bw Jackson
Audiface, Maonyesho hayo ya aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye
lengo la Kuzitangaza Kazi za Vijana Wajasiriamali .
“Maonyesho
haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili
Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za
Ujasiriamalia.
Aliongeza
kuwa washiriki watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu
Mbalimbali na Namna Ya Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa
Wingi zaidi.Namna ya Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara
Kutoka Mamlaka Mbalimbali za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha
Bidhaa zao ziendane na soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya
Wateja.Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu
namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza
mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema
Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina
pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.
Washiriki
wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha
Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya
Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa
hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali
Wanazofanya Vijana. Pili kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma
zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda.
0 comments:
Post a Comment