MANISPAA YA KINONDONI YAPITISHA BAJETI YA SHS.BILIONI 121



Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti ya sh.bilioni 121 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Yusuph Mwenda alisema fedha hizo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya mapato , pesa kutoka ruzuku serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo ya ndani ya Halmashauri .Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa kujiendesha kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa ikijiendesha kwa asilimia 20 tu.

Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo la kutekeleza mipango ya maendeleo na kuwaondolea umaskini wakazi wa kinondoni na kuboresha maisha yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni.
Dj sek blog
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: