Baadhi
ya Wanajumuiya ya Watazania waishio Mjini Seattle – Washington Nchini
Marekani ambao walikuwa katika tafrija ya pamoja na Ujumbe wa Kiserikali
wa Zanzibar uliokuwa mjini humo kushiriki Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika wa Mji Huo ukiongozwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi
ya Wanajumuiya ya Watazania waishio Mjini Seattle – Washington Nchini
Marekani ambao walikuwa katika tafrija ya pamoja na Ujumbe wa Kiserikali
wa Zanzibar uliokuwa mjini humo kushiriki Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika wa Mji Huo ukiongozwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi
ya Wanajumuiya ya Watazania waishio Mjini Seattle – Washington Nchini
Marekani ambao walikuwa katika tafrija ya pamoja na Ujumbe wa Kiserikali
wa Zanzibar uliokuwa mjini humo kushiriki Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika wa Mji Huo ukiongozwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi
ya Wanajumuiya ya Watazania waishio Mjini Seattle – Washington Nchini
Marekani ambao walikuwa katika tafrija ya pamoja na Ujumbe wa Kiserikali
wa Zanzibar uliokuwa mjini humo kushiriki Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika wa Mji Huo ukiongozwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Najisikia
raha kupiga picha ya pamoja na wajukuu zangu. Alijikuta akitamka maneno
hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya
kuwahutubia Wanajumuiya ya Watanzania waishio Mji wa Seattle Nchini
Marekani kwenye tafrija aliyoandaliwa yeye na ujumbe wake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwaasa Wanajumiya ya
Watanzania wanaoishi Seattle kukumbuka hatma ya maisha yao ya baadaye
kwa kuwekeza nyumbani.
Mtoto
Hanan Masoud Kayanda wa familia za Wanajumiya ya Watanzania wanaoishi
Seattle akimuuliza swali Balozi Seif kuhusu masuala ya Elimu Zanzibar
ambalo lilijibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Nd. Abdulla
Mzee Abdulla aliyekuwemo pia kwenye ujumbe wa Zanzibar uliozuru Mji huo
wa Kifahari.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi maalum kutoka
kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Seattle Nd. Yona
Isimika kwenye tafrija aliyoandaliwa na Ujumbe wake Mjini Seattle. Kati kati yao ni Meneja Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited { PBZ } Juma Amour Mohammed.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wana kamati ya maandalizi ya Tafrika aliyoandaliwa yeye na ujumbe wake ya Jumuiya ya Watanzania waishio Seattle
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud
Mohammed hakuwa mbali katika kupiga picha ya pamoja na baadhi ya
wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi Seattle Nchini Marekani. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
|
------------------------------------------------
Watanzania
waishio na kuendesha maisha yao Nchini Marekani wameawa kuwa makini
katika kuutumia vyema muda wao wa maisha Nchini humo kwa
kufikiria mbinu za kujiwekea mitaji itakaowajengea hatma njema hapo
baadaye endapo watafikia maamuzi ya kurejea kuishi nyumbani siku zijazo.
Nasaha
hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi
katika Mji wa Seattle ndani ya Jimbo la Washington kwenye tafrija maalum
iliyoandaliwa na wana jumuiya hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli
ya Ramada Tukwila Mjini Seattle.
Balozi
Seif alisema wapo baadhi ya Watanzania waliobahatika kupata fursa na
nafasi nzuri za kuendesha maisha katika Mataifa mbali mbali ya nje
hasa ya ulaya lakini wengi kati yao wameishia kuwa na maisha mabovu kwa
kukosa kujiwekea misingi mizuri.
Alisema
tabia ya kuendelea na kuendekeza starehe sambamba na matumizi ya
kifahari kwa msingi wa kutaka sifa hutoa sura mbaya kwao lakini
kinachoumiza zaidi ni kile kizazi chao kinachowategemea.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wana Jumuiya hiyo ya Watanzania
wanaoshi Mjini Seattle kuzingatia na kuheshimu sheria na taratibu za
nchi wanayoishi ili kulinda desturi na ukarimu walionao.
Amewapongeza
wana jumuiya hiyo ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle kwa umoja na
ushirikiano waliokuwa nao bila ya mgongano na ubaguzi wa uzawa ambao
ndio utanaowasaidia katika kuimarisha mila na silka zao.
“
Ukweli sifa tulizokuwa nazo sisi Watanzania hatufanani na wenzetu wa
mataifa mengine . Hivyo Utanzania wetu ni vyema tukauendeleza kwa
kusaidiana na ofisi za balozi zetu zilizo karibu “. Alisisitiza Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Akijibu
baadhi ya maswali alioulizwa na Wanajumuiya hiyo ya Watanzania waishio
Mjini Seattle Balozi Seif aliwatoa hofu wanajumiya hao kwa kuwaeleza
kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hivi sasa inaendelea kuwa shwari
licha ya vituko vinavyotokea katika baadhi ya wakati hasa vile
vilivyokuwa vikiwatia hofu wananchi vya kumwagiwa watu tindikali.
Alieleza
kwamba Serikali iko makini katika kuhakikisha vitendo vya uvunjaji wa
amani havipewi nafasi na tayari vyombo vya ulinzi vinaendelea na
operesheni za kuwasaka watu wenye tabia kama hizo zinayotishia maisha ya
Jamii.
Akijibu
swala la operesheni kimbunga iliyowakumba watu waliokuwa wakiishi
kinyume na taratibu za uhamiaji Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali iliamua kufanya operesheni hiyo
baada ya kugundua wahamiaji haramu ndio wanaohusika na masuala ya
ujambazi Nchini.
Alifahamisha
kwamba watu wote walioondoshwa Nchini Tanzania kupitia operesheni
Kimbunga hiyo wamebainika kutokuwa na kibali jambo ambalo ni kosa
kwa mujibu wa mfumo na taratibu za uhamiaji Kimataifa.
Hata
hivyo Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kuheshimu haki za Binaadamu haijamkataza mtu wa nchi
yoyote Duniani kuishi Tanzania endapo atazingatia sheria za Nchi
zilizopo.
“
Serikali imelazimika kuwa makini katika kulinda usalama wa wananchi
baada ya kugundua kwamba wengi wa wahamiaji haramu ndio waliokuwa
wakihusika katika masuala ya ujambazi na matukio ya hatari hapa Nchini
“. Alisema Balozi Seif.
Wakitoa
salamu zao kwa wanajumiya hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui wamewashauri wanajumuiya hao
kuzitumia fursa za mitaji zilizopo nchini humo kwa kuanzisha miradi
Nchini Tanzania.
Mawaziri
hao walisema mitaji hiyo ambayo fedha zake hazina masharti makubwa
zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ajira hasa kwa vijana pamoja na
kuongeza vipato vyao vitakavyopunguza umaskini.
Walieleza
kwamba wanajumiya hayo ni vyema wakaitumia Diasfora wakielewa kwamba
Tanzania ni yao na kwame bila ya wao hakutakuwa na mgeni atakayeweza
kuweka misingi ya kuimarisha uchumi wa taifa.
Mapema
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle Jimboni
Washington Nchini Marekani Nd. Yona Isimika alisema jumuiya yao
iliyoanzishwa mwaka 2008 hivi sasa ina karibu wanachama Mia Nne.
Nd.
Yona alisema Jumuiya yao iliyolenga kuuendeleza Utamaduni, Mila na
Silka zao za Kitanzania iko katika mchakato wa kubadilisha katiba ili
ikidhi matihaji yao hasa wakati wanapopatwa na matatizo.
Mwenyekiti
huyo wa Jumuiya ya Watanzania waoishi Seattle Washington alipongeza
Ujumbe huo wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwa hatua yake ya kukutana nao ikiwa ni ugeni wa mwanzo tokea
kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 2008.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
11/11/2013.
0 comments:
Post a Comment