PICHA MBALI MBALI : ZIARA YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) BW. LUDOVICK UTOUH KATIKA UKAGUZI WA UMOJA WA MATAIFA.

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.

 Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15 zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).
 Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China)
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen  Clark Mtendaji Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na menejimenti ya shirika hilo.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa UN Women Bi. Lakshmi Puri (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Ludovick S. L. Utouh mara baada ya kikao cha pamoja cha kilichofanyika makao makuu ya Ofisi, mjini New York Marekani.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tuvako Manongi (Watatu Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania, New York Marekani.
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: