Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV.
Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO
la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha
siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi
jumamosi hii januari 30 mwaka huu mjini Dodoma.
Mbio
hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon
ambazo zitashirikisha washiriki mbali mbali wakiwamo waheshimiwa
wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.
Akizindua
mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya
JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la
kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho
hilo ni kufufua michezo hapa nchini.
Pia
alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe
Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa
februari 14 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu
ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha
wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.
Mbio
za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote
na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi
watapata zawadi .
Akitangaza zawadi kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na
wanawake
atapata zawadi ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa
pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000
huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.
Mshindi
wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja
huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ndiye atayakuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki mbio za kilomita 2.5.
Wanafunzi
waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio
wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni
kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka
zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.
Uzinduzi
huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi
vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil
mapema mwezi Agosti mwaka huu ambako nchi zaidi ya 216 kutoka kila
kona ya dunia zitashiriki.
Wanariadha
hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa
2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na
watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya
majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.
Julai
6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini
Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za
Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana na kumaliza katika nafasi ya
nne.
|
0 comments:
Post a Comment