Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura (Kulia) akimkabidhi cheti
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa(TTCL) Justine
Mwandu(Kushoto) baada ya kukamilisha mradi wa kuunganisha Makao Makuu ya
NIC na matawi 24 nchi nzima kwenye mtandao wa TTCL(MPLS-VPN). Tukio
hilo limefanyika katika ofisi za Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Meneja
wa Mradi wa TTCL Ngayalina Mihayo akitoa ufafanuzi kuhusu Shirika la
Bima la Taifa jinsi lilivyounganishwa katika mtandaowa TTCL wa MPLS-
VPN.
NIC and TTCL wakiwa katika picha ya pamoja
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mauzo wa TTCL Peter Ngota (Kulia) akiteta jambo na
Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,Sam Kamanga
(Kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Justine Mwandu (Kushoto) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu
wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura (Kulia) kwenye halfa fupi ambayo TTCL
ilikuwa ikikabidhi mradi baada ya kukamilika wa MPLS VPN over Fibre
Connectivity.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limekabidhiwa mradi wa kuunganisha ofisi ya Makao Makuu na Matawi yake 24 yaliyopo nchi nzima pamoja na makao makuu ya NIC kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ambapo mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 170 za kitanzania.
Ofisi zilizounganishwa na Mkongo wa Taifa ni pamoja na Makao Makuu ya NIC yaliyopo Dar es salaam kwenye makutano ya barabara ya Pamba na mtaa wa Samora, NIC ina matawi manne Dar-es-Salaam ambayo ni: Tawi la City lililopo jengo la Bima la kitega uchumi; Tawi la Life House lililopo mtaa wa Sokoine; Tawi la Kisutu lililopo Kisutu; na Tawi la Ubungo, lililopo jengo la Ubungo Plaza, Ubungo. Matawi mengine ni Arusha, Kibaha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Singida, Songea, Sumbawanga, Tabora, Tanga, na Zanzibar.
Kutekelezwa kwa mradi huu, pamoja na kusimikwa kwa mfumo mpya wa Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) uliokamilishwa hivi karibuni, kutatoa fursa ya NIC kutoa huduma kwa wateja wake kwa ufanisi na uhakika zaidi. Awali taarifa za wateja kutoka tawi mmoja kwenda makao makuu au tawi jingine ilikuwa ikuchukua muda kushughulikiwa, lakini kuja kwa teknolojia hii itasaidia katika kufikisha taarifa za wateja kwa haraka zaidi na kushughulikiwa kwa haraka. Aidha, Shirika la Bima la Taifa litaongeza ufanisi katika utendaji wake wa kazi ikiwa na pamoja masuala yote yanayohusu kampuni kuwa katika mfumo wa kielektroniki.
Kuingia kwenye huduma hii ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupitia TTCL tunategemea kuongeza uzalishaji zaidi, kwani sasa tunaweza kuhudumia wateja wengi kwa wakati mmoja na kwa haraka zaidi. Lengo letu ni kuhakikisha tunawafikia na kuwapa huduma ya bima watanzania wengi waliopo mjini na vijijini.
Aidha, taarifa za wateja zitakuwa kwenye mfumo wa kielektroniki ambapo itatoa wepesi katika kushughulikia madai na maombi ya wateja. Hatua hii itaiweka NIC kuwa kinara katika matumizi ya TEHAMA kwenye kutoa huduma ya bima kwa wateja wake nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.
Katika mradi huu pia, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) itatoa huduma ya intaneti, na mfumo wa kutuma na kupokea taarifa kwa kitaalamu (Mult-Protocol Label Switching -Virtual Private Network- MPLS VPN) ambapo NIC itafaidika na intaneti yenye ubora, pamoja usalama wa kutuma na kupokea taarifa za wateja wake na za kampuni kwa ujumla.
Kwa sasa Shirika la Bima la Taifa liko kwenye hatua kubwa ya utekelezaji wa mageuzi ya kibiashara yenye lengo kuboresha huduma zake kulingana na Mpango wake wa Biashara (NIC Business Plan 2013 – 2016).
0 comments:
Post a Comment