Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin
Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa
uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama JayMillions
itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali
zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja
anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila
siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia
ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Balozi
wa promosheni ya JayMilions Hilary Daud ”Zembwela” (kushoto) akionesha
bango linaloelezea jinsi ya mteja kujua kama ameshinda katika Promosheni
hiyo iliyozinduliwa na Vodacom Tanzania leo itakayowawezesha wateja wa
kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi
Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu
kila siku yenye neno “JAY” kwenda namba 15544.Wengine kutoka kulia
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Mkuu wa
Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Vodacom
imezindua promosheni kubwa kuliko zote katika historia ya michezo ya
bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja watajishindia pesa taslimu
Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha siku 100.
Akizungumza
na waandishi wa habari jjijini leo ,Mtendaji Mkuu wa Vodacom
Tanzania Rene Meza amesema promosheni hii inajulikana kama JayMillions
na inawahusisha wateja wote wa Vodacom na ni ya kwanza ya aina yake
kwani, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa
kila mtu kushiriki.”
Vodacom
itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na
washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi
elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-
kila siku.
Meza
ameongeza kuwa hii inadhihirisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na
kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha
ya wateja kuwa murua zaidi “ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na
familia ya Vodacom kila siku.”
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa
amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom,
aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY”
kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la. Mara tu
ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama
ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa
ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.
“”Tofauti
na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki. Tuma
ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi,
wala chemsha bongo na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi
kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku
unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.
Alisema
kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa
promosheni hii. “Ili kujua kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda
kukusisitizia mteja wetu kutuma ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda
15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa.
Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua
kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila
siku,” alisisitiza Twissa.
0 comments:
Post a Comment