Dereva
Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(katikati)Akizungumza na
Wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani
Mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance
Autos,Kulia ni Meneja mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne Mcintosh na
kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(Wa Kwanza Kulia)akiwaelezea
jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa
Alliance Autos Tharaia Ahmed
Meneja
mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne Mcintosh akielezea ni kwa namna
gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea gari ya Volsk
Wagen Aliyosafiri nayo Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer
Zietlof(Martha Magessa)
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva
Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya
gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi
zaidi ya 19 Duniani
Dereva
Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari
yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi
zaidi ya 19 Duniani
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu
ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg
V6 TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani
Dereva
Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance
Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja
na wanahabari
Meneja Mkuu wa Alliance Autos Wayne Mcintosh(kushoto) Akipata picha na Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed(kushoto)akipata picha na Dereva Rainer Zietlof
Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka ujerumani
-----------------------------------------
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya
dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo
itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka
2011 na 2012.
Awali
alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama 'Panamerica'ambayo
ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17
wakati ile ya 'Russtralia' ilimtoa Melbourne, Australia hadi
St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof
anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake
Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia
kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa
17,000.
Kwa
mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za
Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia,
Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na
sasa Tanzania.
Dereva
huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance
Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa
atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji
nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha,
amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira
tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na
barabara mbovu.
Mradi
huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa
na makampuni makubwa ya magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani,
Slovakia na Afrika Kusini.
Katika
safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye
ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa
mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
0 comments:
Post a Comment