Prof. Reuben Mwamakimbullah kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
(SUA) akionesha kwa vitendo namna kuangalia maji kwenye nguzo kwa kutumia kifaa
kinachoitwa ‘Electrical Resistance Metter’.
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Iringa Mhandisi Seraphine Lyimo akifungua mafunzo hayo awamu ya pili.
Msimamizi wa mafunzo hayo Meneja wa Kitengo cha Usalama Kazini ambao ndio waandaji Mhandisi Majige Mabulla akiwakaribisha washiriki na kuelezea namna ambavyo mafunzo hayo yataendeshwa kwa nadharia na vitendo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Iringa Mhandisi Seraphine Lyimo akifungua mafunzo hayo awamu ya pili.
Msimamizi wa mafunzo hayo Meneja wa Kitengo cha Usalama Kazini ambao ndio waandaji Mhandisi Majige Mabulla akiwakaribisha washiriki na kuelezea namna ambavyo mafunzo hayo yataendeshwa kwa nadharia na vitendo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini
Na Henry Kilasila, Iringa
Wahandisi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO)
wameanza kunolewa katika kutambua nguzo bora za kusambazia umeme majumbani
katika kukabiliana na matumizi ya nguzo zisizo na ubora na ili kuongeza ufanisi
na usalama katika zoezi la kusambaza umeme nchini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yanayofanyika mkoani
Iringa kujumuisha wahandisi wakuu wa umeme, maafisa mipango na maafisa usalama
wa TANESCO yana lengo la kuwawezesha wataalamu hawa kuwa na weledi wa hali ya
juu katika kutambua nguzo zenye sifa na umadhubuti na salama katika zoezi la
usambazaji umeme nchini.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Mkoa wa Iringa
Mhandisi Seraphine Lyimo alisema
anaamini mafunzo haya yatawawezesha washiriki kufanya vizuri zaidi katika
utendaji wao wa kazi na kuongeza kuwa Shirika halitapata tena nguzo ambazo
hazina viwango na kuwataka washiriki kuendelea kujisomea zaidi na kuzielewa
nguzo ili kuokoa rasilimali chache za Shirika.
Mhandisi Lyimo aliongeza kuwa mafunzo
hayo yana faida kubwa kwa TANESCO kwani yatasaidia Shirika kuepuka kununua
nguzo feki na hivyo kuweza kuliepushia Shirika hasara zisizo za lazima.
“Nawaomba muzingatie mafunzo haya ili muje kutumia
utaalamu huu katika kulisaidia Shirika wakati wa manunuzi ili kuweza kuwapatia
Watanzania huduma bora na salama ili kukidhi kiu yao ya hupatikanaji wa umeme,”
alisema Mhandisi Lyimo.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Prof. Reuben Mwamakimbullah kutoka Chuo Kikuu
cha Kilimo (SUA), alisema kuwa baadhi ya vitu vinavyochangia kuharibu ubora
wa nguzo ni pamoja na kutoboa nguzo matundu wakati imeshawekewa dawa; na
kuongeza kuwa maji nayo huchangia kuzuia
uwezo wa dawa kupenya kwenye nguzo na ujazo wa hewa ndani ya nguzo ambayo
inatakiwa nayo itolewe ili dawa iweze kupata nafasi.
Prof. Mwamakimbullah aliwasihi washiriki wa mafunzo
hayo kuwa waangalifu katika utambuzi wa nguzo za matumizi ili kuokoa uwezekano
wa kuhatarisha maisha ya watumiaji na pia kuliokolea Shirika hasara.
“Nawaomba
muzingatie ubora wa nguzo kwa kuzingatia
unaandaaje nguzo zako, unatumia dawa gani na unatumia njia gani kuingiza dawa
katika nguzo,” aliwasihi Prof.
Mwamakimbullah.
Prof. Mwamakimbullah aliwataka washiriki
kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana akiwasihi ili kufikia malengo ya
Shirika wataalamu hao hawana budi kushirikiana na wengine ili kuwezesha TANESCO
huduma bora na bidhaa bora.
Naye msimamizi wa
mafunzo hayo Meneja wa kitengo cha usalama kazini wa
TANESCO, ambao ndio waandaji Mhandisi Majige Mabulla alisema: “Tunategemea kuona ufanisi katika utendaji
kutokana na mafunzo haya mkayoyapata, kwa faida ya kwako mshiriki na pia kwa
faida ya Shirika.”
Kwa
mujibu wa taratibu za usalama, nguzo inatakiwa kwa kawaida ikae sio chini ya
miaka 40 na takwimu zinaonesha kuwa nguzo zisizo na ubora kwa wastani wa
hazifiki miaka zaidi ya saba.
0 comments:
Post a Comment