Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt Shaibu Shehe
Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa ni miongoni mwa
wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa hivi karibuni
Nchini Sudan Jimbo la Darfur.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika Hitma
ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan
hivi karibuni,Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma
Ally iliyosomwa katika msikiti Masjid NuruMuhammad,Mombasa Mjini Unguja
leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika
kuwaswalia Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally
,mbele katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja
leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan
hivi karibuni.
Wanajeshi
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa
Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya kuwasilim katika makaburi ya
Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7
waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi
karibuni.
Baadhi
ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa
marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika
katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa
leo,mchana.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) na Vingozi na Waislamu,wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi
la Ulinzi la Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu
Sgt Shaibu Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya
Mwanakwerekwe leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
0 comments:
Post a Comment