Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali
na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma
akizungumza na wandishi wa habari (pichani hawapo), katika mkutano wa
nne wa mafunzo ya upasuaji wa ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya
fahamu Dar es Salaam leo. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid, unao endelea hadi Mei 15-2015. (PICHA
ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba MOI, Dk. Abednego Kinasha akitoa mada katika mkutano huo
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (watatu kushoto),
akitetajambo na madaktari hao baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar
es Salaam leo unao endelea hadi Mei 15-2015 , (wa kwanza kulia) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali
na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma,
wakwanza kushoto ni Daktari Bingwa wa Taasisi hiyo, Anthon Assey na
anaye fatia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na
mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (kushoto)
akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha na Ugavi katika Taasisi ya Tiba ya
Mifupa, Ajali
na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Kevin Felix
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif (kushoto) Rashid akisalimiana na Profesa J. Kahamba
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (kulia) akisalimiana
na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu katika Taasisi ya Mifupa Moi
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (kulia) akisalimiana na
Mkurugenzi wa Uuguzi katika taasisi ya mifupa Moi Flora Kimaro baada ya
kufungua mkutano wa
nne wa mafunzo ya upasuaji wa ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya
fahamu Dar es Salaam leo
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid katika picha ya pamoja na maktari hao
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (watatu kulia) katika picha
ya pamoja baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam leo
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid (watatu kushoto) akiwa na
madaktari, wakurugenzi na maprofesa kutoka New york katika chuo cha
weill Cornell na New York Presbyterian Hospital
Madaktari wakiwa katika mkutano huo
Madaktari na baadhi ya wakuu wa vitengo wakisikiliza kwa umakini wakati mada mbalimbali zilikuwa zikitolewa
wakisikiliza kwa utulivu mkubwa madaktari hao
madaktari mbalimbali wakutoka sehemu tofauti wakiwa katika mkutano huo
Profesa Philip stieg, kutoka New york katika chuo cha weill Cornell na New York Presbyterian Hospital akiongea na waandishi wa habari (pichani hawapo) baada ya kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif Rashid
Madaktari wa magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo mbele wakiwa na washiriki katika mkutano huo
Salha Mohamed
SERIKALI imesema inaupungufu wa madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo.
Yalibainishwa hayo Dar es Salaam leo, na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid wakati wa mkutano wa madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo na uti wa mgongo waliotoka nchi za Marekani, Ujerumani, Hispania, Uturuki pamoja na Misri na wakishirikiana na madaktari mbalimbali wa Tanzania.
SERIKALI imesema inaupungufu wa madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo.
Yalibainishwa hayo Dar es Salaam leo, na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid wakati wa mkutano wa madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo na uti wa mgongo waliotoka nchi za Marekani, Ujerumani, Hispania, Uturuki pamoja na Misri na wakishirikiana na madaktari mbalimbali wa Tanzania.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuongeza taaluma na kubadilishana uzoefu miongoni mwa madaktari hao bingwa katika mishipa ya fahamu, ubongo na uti wa mgongo kwenye upasuaji.
"Hili ni eneo muhimu sana, kwani magonjwa haya yanaongezeka sana ikiwa ni kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa ya ajali na maradhi yanayopelekea kupata matatizo katika mishipa hiyo," Dk Rashid.
Alisema mkutano huo utawawezesha kufanya kazi kwa umakini na upatikanaji wa vifaa vya kutolea huduma hiyo ili kuweza kuongeza uwezo mkubwa zaidi katika upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa mafanikio makubwa zaidi na kuweka mwelekeo mzuri wa kazi hiyo kwa urahisi zaidi.
Aidha alisema changamoto ya madaktari bingwa ni kubwa zaidi kuliko uwepo wa madaktari hao ambapo wanahitajika zaidi katika taaluma hiyo.
"Juhudi za kutoa fursa kwa madaktari hao ni ndogo kwani bado linahitajio kubwa kwasababu ya mabadiliko ambapo kila siku ajali zimekuwa zikiongezeka," alisema huku akisema zaidi ya asilimia 25 ya wagonjwa ya fahamu na ubongo na uti wa mgongo yanatokana na ajali.
Aidha alisema jengo la Moi litazinduliwa kabla ya uchaguzi ambapo lipo kwenye hatua ya mwisho na kwamba vifaa vitafika baada ya muda mfupi na lipo kwenye hatua za mwisho.
"Jengo hilo jipya litazinduliwa kabla ya uchaguzi mkuu ambapo limekamilika kwa asilimia 90, na litakuwa na vitanda 240 na eneo la kuwezesha wataalamu kutoa huduma bila changamoto zozote.
0 comments:
Post a Comment