SAKATA LA UVCCM ARUSHA LAUNDIWA KAMATI ILI KUPATA MUAFAKA

Katibu mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda akiongea katika moja ya ziara yake Mkoani Arusha hivi karibuni  ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi kufanya Mkoani hapa
 *********
SAKATA la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha sasa kupatiwa muarubaini wake ambapo  imedaiwa kuundwa timu maalumu itakayochunguza mgogoro huo. 
 
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda ameeleza mtandao wa jamiiblog kuwa kutokana na kinachoendelea hivi sasa katika umoja wa vijana Mkoa wa Arusha kuwa tayari Makao makuu wameshatuma timu ya kuchunguza mgogoro huo
 
Alisema kuwa tayari timu hiyo imeshawasili jijini Arusha hivyo kuanza kazi rasmi kesho (leo)itakayopelekea kubaini ni nini hasa chanzo cha mgogoro huo ambao unaendelea katika umoja huo wa vijana
 
“Taarifa za kinachoendelea Arusha katika umoja wa vijana tayari ila tumeshatuma timu maalumu ya kuchunguza ni nini hasa kinasababisha vurugu hizo”Alisema Mapunda
 
Aidha Mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku ameshangazwa na utaratibu uliotumika kuwaita katika kikao cha Sekretarieti unaotarajiwa kufanyika kesho ambapo alidai wajumbe walitumiwa mualiko kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno(sms)
 
Kuhusu kikao cha kesho (leo) kilichoitwisha na Sekretarieti ya mkoa chini ya Katibu wake Mary Chatanda, mwenyekiti Meitinyiku alisema utaratibu uliofanyika kuwajulisha wajumbe kuhusu kikao hicho ni wa ‘kihuni’ kwa kuwa walitumiwa taarifa kwa ujumbe wa simu badala ya kujulishwa kwa barua kama inavyotakiwa.
 
 “Nashangaa kwa kweli nimetumiwa ujumbe mfupi wa maneno na Gerald Mwadalu tuliyemsimamisha kuwa kesho kutakuwepo na mkutano wa sekretarieti ya Mkoa sijajua kikao hicho kitahusu nini hasa ila pamoja na hayo haizuii mimi kutohudhuria”alisema Meitinyiku
.
Aidha alisisitiza kikao walichokifanyacha baraza la vijana mkoa na  kuwatimua Katibu wa UVCCM Mkoa Gerald Mwadalu kilikuwa sahihi licha ya kudaiwa kuwa kilikuwa kikao feki kwa kuwa idadi ya wajumbe walikuwa wametimia
 
Mwadalu akizungumza jana alisema kuwa kila kitu kitajulikana kwenye kikao cha (leo) cha Sekretarieti ya Mkoa kwamba hawa wanapata wapi nguvu za kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na taratibu za umoja wa vijana.
 
Kwa sasa aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa muda Daniel Kayongo kutoka Longido
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: