KONGAMANO LA NNE LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA (TAPSEA) LAFUNGULIWA JIJINI MWANZA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.

Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Kisheria wa TAPSEA,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mh. Amina Masenzo akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo,uliofanyika leo jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza
Meza Kuu.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu pamoja na Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki wakati wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania, Julai 11,2013 jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Bhoke Matinyi akitoa taarifa ya Chama kwenye Kongamano hilo lililofunguliwa leo jijini Mwanza.
MC. Angella Bondo akiwajibika.
MC. Ephrahim Kibonde.
Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.
Picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa TAPSEA.
Picha ya pamoja na Baadhi ya Wadau wa Kongamano hilo. Picha Zote Na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: