UBALOZI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE) WASHEREHEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50 MUUNGANO WA TANZANIA

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu,Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) akimpokea mgeni rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano Tanzania, Mheshimiwa Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa UAE,katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Intercontinental,Abu Dhabi..
Balozi Mbarouk akiwa na Chief of Protocol wa UAE Mhe. Shihab Al Faheem.
Balozi Mbarouk akimuongoza Mgeni rasmi Mhe. Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na Mabalozi wanao wakilisha nchi zao hapa UAE kuingia katika ukumbi wa Sherehe.
Balozi Mbarouk na Mama Balozi wakipokea wageni waalikwa
Mhe. Balozi, Mgeni Rasmi na baadhi ya Mabalozi wanao wakilisha nchi zao nchini UAE, wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za UAE na Tanzania

Balozi Mbarouk akitoa hotuba katika sherehe hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa, akiwepo Mhe. Mallallah Mubarak (mwenye kilemba cheupe), aliyewahi kuwa Balozi wa UAE nchini Tanzania.
Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omary Mjenga akiwa na familia yake na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi.
Wageni waalikwa wakipata chakula.
Balozi Mbarouk akiwa na wachezaji mashuhuri wa zamani wa timu za Yanga, simba na Timu ya Taifa, Alluu Ally, Omar Hussein na Yanga Bwanga wanaoishi nchini UAE.
Watanzania wanaoishi nchini UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na viongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi Mdogo Bw. Omary Mjenga akiwa pamoja Mwenyekiti wa Watanzania nchini UAE Bw. Mohammed Sharif na wageni waalikwa.
Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

0 comments: