DKT. GHARIB BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA 12 AFRIKA NCHINI ABUJA,NIGERIA.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mfalme Mswati (ii) wakati walipokutana kwenye Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Katikati yao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, leo  mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Mahadhi, wakisimama wakati zikipigwa nyimmbo za Taifa ukumbini humo.
 Rais wa Nigeria, Gudluck Jonathan (kulia) akiongozana na baadhi ya marais, wakati akiwasili ukumbini hapo kufungua rasmi mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.Picha Kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: