Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji,
lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa
Tanga leo, Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku
Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya
Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia
amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni. Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati
akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani
Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na
kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
0 comments:
Post a Comment